TEHRAN: Iran sasa itaendelea na mpango wake wa nuklia.
28 Februari 2005Matangazo
Iran na Urusi zimetia saini mkataba wa nuklia ambao sasa Urusi itaipa Iran malighafi za Nuklia.
Kutiwa saini mkataba huo kunaipa Iran nafasi ya kutekeleza ujenzi wa kituo chake cha kwanza cha nguvu za atomiki huko Bushehr.-
Katika mkataba huu Iran itarudisha mabaki yote ya chembechembe za mafuta kwa Urusi, ili kukinga uwezekano wa kutengeneza silaha za kinuklia.
Hatua hii ya Urusi kutia saini mkataba wa nuklia na Iran umeikasirisha Marekani na maseneta mjini Washington wameitaka serikali ya rais Bush kuichukulia Urusi hatua kali ikiwemo kuondolewa uanachama wake kutoka kwa baraza la mataifa manane yenye uwezo wa kiviwanda G8.
Iran inasisitiza kuwa mpango wake wa nuklia hauna nia ya kuleta madhara yoyote.