TEHRAN. Iran kufikishwa mbele ya baraza la usalama la umoja wa matifa
13 Julai 2006Nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani zimepitisha uamuzi wa kuifikisha Iran mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Hatua hiyo imeafikiwa baada ya Iran kukataa kusimamisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank- Walter Steimier amesema kwamba Iran sasa itakabiliwa na vikwazo.
Steinmier aliyasema hayo baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za umoja wa ulaya uliofanyika mjini Paris Ufaransa.
Wawakilishi wa nchi za umoja wa ulaya wamesema kwamba wana hofu kuwa mpango wa mapendekezo ya vivutio kwa Iran hautafanikiwa baada ya kumalizika kwa mkutano wao na mpatanishi wa maswala ya nyuklia wa Iran Ali Ralijani.
Nchi za magharibi zinahofia kuwa huenda Iran ina azimia kutengeneza silaha za kinyuklia.