TEHRAN: Iran inatakiwa kutoa ushirikiano katika uchunguzi dhidi yake.
1 Machi 2005Matangazo
Mkurugenzi wa kuangalia mipango ya nuklia wa Umoja wa Mataifa Mohamed el Baradei ameitaka Tehran ishirikiane zaidi katika uchunguzi dhidi Iran kwamba inahusika na mpango wa kutengeneza silaha za kinuklia.
Alitoa agizo hilo katika mkutano wa kamati maalum unaoendelea huko Vienna.
Urusi bado inatetea hatua yake ya kutia saini mkataba wa kuipa Iran Malighafi za nuklia katika kituo chake kipya cha nguvu za atomiki cha Bushehr.
Mkuu wa shirika la nguvu za atomiki wa Urusi Alexandar Rumyantsev amesema kuwa Urusi itaipa Iran malighafi za nuklia lakini itahakikisha kuwa Iran haitumii chembechembe za mabaki ya mafuta kutengeneza silaha za kinuklia.
Marekani inapinga hatua ya Urusi ya kujihusisha katika mpango huo.