Tehran. Iran iko tayari kujadiliana na mataifa ya Ulaya.
20 Agosti 2005Iran iko tayari kuangalia mapendekezo yeyote mapya ya umoja wa Ulaya yenye lengo la kutatua mzozo juu ya shughuli za taifa hilo za kinuklia lakini haitarejea tena katika kusitisha kabisa shughuli zake.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Iran Hamid Reza Asefi amewaambia waandishi wa habari kuwa ni kawaida iwapo umoja wa Ulaya utabadili mapendekezo yake, na katika mapendekezo hayo mapya itatambua haki ya taifa hilo la Kiislamu , hapo ndio mapendekezo hayo yataangaliwa.
Lakini ameongeza kuwa Iran inataka kujadiliana lakini bila kuwekewa masharti kabla.
Iran imeingia katika mzozo na jumuiya ya kimataifa baada ya kuanza tena shughuli za kuyabadili madini ya Uranium , ambayo ni hatua ya kwanza ya kuelekea kurutubisha madini hayo, katika kinu chake kilichoko Isfahan mapema mwezi huu.