TEHERAN: Rais wa Iran atuma barua kwa Kansela Merkel
20 Julai 2006Matangazo
Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amewasiliana na Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel kwa njia ya barua.Ubalozi wa Ujerumani mjini Teheran umethibitisha hayo.Yale yaliyokuwemo katika barua hiyo bado haijulikani.Ujerumani,pamoja na Uingereza na Ufaransa tangu miezi kadhaa inajaribu kusuluhisha mgogoro unaohusika na mradi wa kinuklia wa Iran.Mnamo mwezi wa Mei,rais Ahmedinejad aliwahi pia kutuma ujumbe kwa rais George W.Bush wa Marekani.Kwa mujibu wa Washington,barua hiyo haikuwa na cho chote kilicho kipya.