TEHERAN: Iran yasema vitisho havitosaidia
16 Julai 2006Iran imesema mpango uliyopendekezwa na madola makuu ya magharibi mwezi uliyopita ni msingi wa kufanywa majadiliano kuhusika na mradi wa kinuklia wa Teheran.Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni,Hamid Reza Asefi alipozungumza mjini Teheran kwenye mkutano wa kila juma pamoja na waandishi wa habari,alitoa mwito kwa viongozi wa madola tajiri yenye viwanda G-8 wanaokutana St.Petersburg nchini Urussi,waamue kufanya majadiliano pamoja na Iran.Akaongezea kuwa vitisho havitofanya kazi na hatua ya kulifikisha suala la Iran mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa haitosaidia.Madola ya magharibi yana khofu kuwa Iran huenda ikawa inajaribu kutengeneza silaha za kinuklia.Iran lakini inasema kuwa mradi wake wa kinuklia ni kwa matumizi ya amani tu.