TEHERAN: Iran na Misri kuanzisha uhusiano wa kibalozi
6 Januari 2004Matangazo
Makamo Rais wa Iran, Bwana Mohamed Ali Abtahi, amesema nchi yake imekubaliana na Misri, kuanzisha uhusiano wa kibalozi, miaka ishirini na tano baada ya nchi hizo kusimamisha uhusiano huo.
Iran ilichukua uamuzi wa kusimamisha uhusiano wa kibalozi na Misri mwaka wa 1979, kupinga uamuzi wa wakuu wa Misri wakati huo, wa kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Israel, na kumukubalia hifadi ya ukimbizi Shah wa Iran.
Makamo rais wa Iran amewaambia waandishi wa habari kwamba wakuu wa Misri na wa Iran wameamua kusahau yaliyopita, na kuanzisha tena uhusiano wa kibalozi. Akasema Misri na Iran zikishirikiana, zinaweza kuwa na ushawishi mkubwa, katika maamuzi yanayohusu siasa za kimataifa.
Wakuu wa Misri hata hivo hawajaelezea chochote kuhusu habari hizo.
Uamuzi huo wa kurejesha uhusiano wa kibalozi baina ya Misri na Iran ikiwa utadhihirika, unafuatia wakuu wa jiji la Teheran kukubali kubadili jina la mtaa mmoja wa jiji hilo, uliopewa jina la mtu alieuwawa Rais wa zamani wa Misri Anuar el Sadate; aliesaini makubaliano ya uhusiano wa kibalozi na Israel. Badala ya jina la mtu huyo, sasa mtu huo utaitwa mtaa wa Intifada-