TEHERAN: Iran haina azma ya kuishambulia Israel
30 Oktoba 2005Matangazo
Iran yadhihirika kurudi nyuma na matamshi yaliotolewa na rais wake kuwa Israel iondolewe kwenye ramani.Hati iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Iran,imesema kuwa Iran inaendelea kujifunga na maadili ya katiba ya Umoja wa Mataifa.Vile vile haina azma ya kuishambulia Israel na itaunga mkono uamuzi utakaopitishwa na Wapalestina kutenzua mgogoro wa Mashariki ya Kati.Matamshi hayo ni tofauti kabisa na hotuba iliyotolewa na rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad siku ya Jumatano.Katika hotuba hiyo alisema Israel “ifutwe kwenye ramani”.Matamshi hayo aliyokariri tena siku ya Ijumaa yaliibua shutuma kutoka sehemu mbali mbali za dunia.