Kaskazini mwa Kenya, kaunti za Turkana na Marsabit zinatatizika kupata maji safi na salama. Maji ya chumvi katika Ziwa Turkana katikati yao yamekuwa si chanzo cha maji ya kunywa na kwamba ni hatari kwa afya za watumiaji. UN inatafuta njia za kuwasaidia watu katika vijiji vinavyotaabika na maji. #kurunzi