Miaka minne sasa tangu salamu hizo za kheri kati ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha upinzani ODM Raila Odinga, yapo mengi yaliyotajwa kuwa mafanikio. Lakini kwa upande mwingine kuna malalamiko kwamba salamu hizo zilisambaratisha uhusiano kati ya rais na naibu wake William Ruto na hata kusababisha migawanyiko zaidi kisiasa.