Tanzania yawarejesha raia waliokuwa Israel
26 Juni 2025Mataifa mengi duniani yaliwahamisha raia wao kutoka Israel na Iran wakihofia maafa ya mapigano yaliyodumu kwa siku 12 na ambayo yalihitimishwa kwa mkataba wa kusitisha vita uliotangazwa mapema wiki hii.
Baadhi ya watanzania walikuwa wakifanya kazi na wanafunzi, na Wazanzibari waliorejea walikwenda Israel kwa ajili ya matibabu, lakini kutokana na vita, Serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na familia na taasisi za kimataifa, imefanikiwa kusaidia kurejea kwao salama.
Wakizungumza huku wakisitasita kutokana na khofu, Hanifa Rashid Abass na Amina Soud waliorejea nyumbani wakitokea nchini Israel wanaelezea wasiwasi waliokuwa nao katika kipindi kigumu cha vita.
"Najisikia vizuri kurudi nyumbani salama pia naishurkuru serikali zetu zote mbili kwa kuturejesha. Tumefurahi tumefika nyumbani salama hali ya kuwa tulikuwa tumeshapoteza matumaini kama tutarudi salama, kwa kweli sio mshituko tu ilikuwa tunaona uhalisia wa mambo. Tulikuwa tunajificha kwenye vyumba maalumu vya kujifichia. Nimejifunza kuwa kuwa na amani ni muhimu kuliko chochote.”
Tanzania imekuwa ikiwapeleka wagonjwa wa moyo Israel
Tanzania imekuwa ikitumia fursa za matibabu ya moyo nchini Israel kwa miaka 26 sasa ambapo bado baadhi ya wagonjwa wapo nchini Israel wakiendelea na matibabu kama anavyothibitisha Daktari Omar Suleiman ambaye anashughulikia kitengo cha maradhi ya moyo Zanzibar.
"Bado tuna wagonjwa 21 na familia za watu 7 wamebaki Israel,” alisema Dkt Suleiman.
Kurejea kwa watanzania hao kumegawanywa makundi mawili ambao kundi moja limerudi moja kwa moja Zanziabr na jengine jijini dare s salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Ali Suleiman Ali uamuzi wa serikali na namna wengine watakavyorudi.
Nchi zote mbili Israel na Iran ni rafiki wa Tanzania na wananchi wamekuwa wakinufaika katika nyanja tofauti kutokana na ushirikiano huo, ikiwemo biashara, watalamu, mafunzo na matibabu lakini vita ni changamoto kwa dunia na ni ujumbe kwetu sote kuthamini amani tuliyo nayo.