Tanzania: Marufuku mazao ya kilimo kutoka Malawi na A.Kusini
24 Aprili 2025Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wake wa Kilimo Hussein Bashe imetangaza kuyapiga marufuku mazao ya kilimo kutoka nchi za Afrika Kusini na Malawi kuingia nchini humo baada ya nchi hizo mbili kuzuia mazao kutoka Tanzania kuingia kwenye nchi zao.
Waziri Bashe ametangaza msimamo huo licha ya kwamba mazungumzo yanaendelea baina ya nchi hizo mbili kupitia kwa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania lakini amesema nchi hiyo haiwezi kuendelea kusubiri na kunyimwa haki hiyo ya kibiashara.
Soma pia: Tanzania: Bashe azuia bidhaa kutoka Malawi na Afrika Kusini
Afrika Kusini imepigwa marufuku kuingiza bidhaa zake za kilimo ikiwemo matunda huku Malawi ikizuiwa kuingiza na kupitisha mazao yoyote ya kilimo nchini Tanzania.
Wiki iliyopita, Tanzania ilitoa taarifa ya kuyataka mataifa hayo kubadili misimamo yao hadi jana siku ya Jumatano na ikaahidi kuchukua hatua hizo ikiwa hayatobadili misimamo yao.