BiasharaTanzania
Tanzania yaondoa marufuku ya uagizaji wa mazao ya kilimo
26 Aprili 2025Matangazo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya na Viuatilifu vya Mimea Tanzania (TPHPA), Joseph Ndunguru amesema jana usiku kwamba, Tanzania inaondoa marufuku hiyo mara moja ili kuruhusu majadiliano ya kidiplomasia ya ngazi ya mawaziri.
Amesema mataifa hayo mawili yamewasiliana na Tanzania kutaka suluhu ya mvutano wa kibiashara kwa njia ya mazungumzo.
Siku ya Jumatano wizara ya kilimo ya Tanzania ilipiga marufuku uagizaji wa mazao yote ya kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini pamoja na usafirishaji wa mbolea ya Tanzania kwenda Malawi ambayo hutegemea sana mbolea hiyo. Zuio la mbolea pia, limeondolewa.