Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lisu ambaye ni mkosoaji wa serikali ya Tanzania, ametiwa mbaroni baada ya kumaliza shuguhuli zake za kimahakama jijini Dar es Salaam. Lissu amewahi kukamatwa mara kadhaa.
M M T/ J3.22.08.2017-Dar Tundu Lissu arrested - MP3-Stereo
Lissu hivi karibuni aliibua sakata la kile alichodai kukamatwa kwa ndege ya Tanzana nchini Canada, kunakotakana na makosa ya kuvunja mkataba kiholela, ambako kumeligharimu taifa hilo takribani shilingi bilioni 87, sawa na dola milioni 38.7 za Kimarekani. DW imezungumza na wakili wake Peter Kibatala na kwanza anaelezea mazingira ya kukamatwa Tundu Lissu.