Tanzania itafungua dimba la CHAN dhidi ya Burkina Faso
28 Juni 2025Wenyeji wenza wa michuano hii, Kenya na Uganda, nao wataanza kampeni baadaye. Kenya, chini ya kocha Benni McCarthy, itashuka dimbani Agosti 3 dhidi ya DR Congo kwenye uwanja wa Kasarani, Nairobi.
Uganda, ambayo haijawahi kufuzu hatua ya mtoano licha ya kushiriki mara sita kati ya saba zilizopita, itakipiga na Algeria Agosti 4 kwenye uwanja wa Mandela National Stadium, Kampala.
Miongoni mwa mabingwa wa zamani watakaoshiriki ni pamoja na DR Congo, Morocco na mabingwa watetezi Senegal. Libya na Tunisia hawatoshiriki wakitaja msongamano wa ratiba za ndani.
Ingawa wachezaji wanaocheza nje ya nchi kama nyota wa Liverpool Mohamed Salah hawatokuwepo, mechi za CHAN zinatambuliwa rasmi kimataifa na zinahesabiwa katika viwango vya dunia vya FIFA.
Mashindano haya pia yanachukuliwa kama maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambalo pia litafanyika kwa pamoja nchini Kenya, Tanzania na Uganda.