Nchi 36 zaidi kuongezwa marufuku ya kuingia Marekani
16 Juni 2025Utawala wa Rais Donald Trump unazingatia kupanua vikwazo vyake vya kusafiri kwa kuwapiga marufuku raia wa nchi 36 zaidi kuingia nchini Marekani. Mapema mwezi huu, rais Trump alitia saini tangazo lililopiga marufuku kuingia kwaraia kutoka nchi 12, akisema anailinda Marekani dhidi ya "magaidi wa kigeni" na vitisho vingine vya kiusalama.
Katika nyaraka ya ndani iliyotiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, wizara hiyo imetaja sababu kadhaa, ikiwemo kukosekana kwa ushirikiano kwa baadhi ya serikali katika kutoa hati za utambulisho zenye kuaminika, kuwaondoa raia wake kutoka Marekani ambao wameamuriwa kuondoka na raia wa nchi hizo kushirki katika vitendo vya kigaidi nchini Marekani.
Tanzania, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni miongoni mwa nchi 36 zinazoweza kukabiliwa na marufuku kamili au kwa kiasi.