Taliban yakataa waranti wa ICC ikisema 'imechochewa kisiasa'
24 Januari 2025Kauli hii inajiri, siku moja baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kusema kuwa anatafuta vibali vya kuwakamata viongozi wakuu wa Taliban nchini Afghanistan kwa unyanyasaji wa wanawake na uhalifu dhidi ya binaadamu.
Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Wizara ya Mambo ya Nje ya Taliban imesema kama maamuzi mengine mengi ya ICC, waranati hiyo haina msingi wa haki wa kisheria.
Mahakama ya ICC yatoa hati ya kukamatwa viongozi wa Taliban
Aidha Taliban imeelezea kusikitishwa na taasisi hiyo ambayo imesema imefumbia macho uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu unaofanywa na vikosi vya kigeni na washirika wao wa ndani wakati wa miaka ishirini nchini Afghanistan.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan, Mohammad Nabi Omari, mfungwa wa zamani wa gereza la Guantanamo Bay, amewaambia waandishi wa habari kwamba ICC haiwezi kuwatisha.