Talanta iliyolelewa katikati ya umaskini mtaa wa Kibera mjini Nairobi imekuwa mwangaza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya kandanda kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17 nchini Kenya. Rebecca Odato aliiwakilisha Kenya, Junior Starlets, katika michuano ya Kombe la Dunia 2024 iliyochezwa nchini Jamhuri ya Dominica. Je, umeiwekeza wapi talanta yako?