Takribani watu 15 wameua mlipuko wa bomu Syria
3 Februari 2025Hayo yameripotiwa na shirika la habari la taifa, SANA, likinukuu vyanzo vya usalama kwenye eneo hilo na shirika linalofuatilia mwenendo wa vita nchini Syria.
Inaarifiwa kwamba gari lililipuka karibu na chombo kingine kilichowabeba wafanyakazi wa mashambani na kuwaua papo hapo wanawake 14 na mwanaume mmoja.
Soma pia:Rais wa Syria awasili Saudia Arabia kwa ziara ya kwanza ya kimataifa tangu kuondolewa kwa Assad
Hata hivyo vyanzo vingine ikiwemo shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria vimesema wanawake 18 na mwanaume mmoja ndiyo wameuawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo.
Mji wa Manbij, kaskazini mashariki mwa jimbo la Allepo bado unashuhudia machafuko hata baada ya kuangushwa kwa utawala wa muda mrefu wa Rais Bashar al-Assad mnamo mwezi Disemba.