Takriban watu milioni 2 hufariki kila mwaka kazini
29 Aprili 2025Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inawategemea vijana katika kulijenga taifa, wengi wa vijana hao hufanya kazi katika mazingira yasiyo salama na kusababisha afya zao kuwa hatarini.
Wafanyakazi wengi wanapuuza suala la usalama kazini
Wamiliki wa makampuni mbalimbali na waajiri na hata watu waliojiajiri hawalitilii maanani suala la afya na usalama kazini.
Waendesha pikipiki, mafundi ujenzi, maseremala, walinzi, wahudumu hotelini na hata wachimba madini wanafanya kazi katika mazingira yasiyo salama.
Hatari zinazowakabili wachimba madini
Katika migodi ya dhahabu ya maala, wachimba madini wameiambia DW kuwa hali ya kazi ni yakutisha na inasababisha maradhi ya mara Kwa mara hata vifo.
Ajali za mara kwa mara kwa wafanyakazi zinapunguza uwezo wa utendaji kazi na kusababisha kuongezeka kwa viwango vya ugonjwa wa muda mrefu.
Mamlaka Tanganyika yawatahadharisha waajiri
Idara ya serikali yenye kusimamia kazi za umma jimboni inakiri kuwepo na viwango vikubwa vya utendaji kazi bila kujali usalama wa wafanyakazi, na kuonya kuwa ni lazima waajiri wawajibike kwa matatizo yoyote yatakayotokea.
Wafanyakazi wachache kunufaika na nyongeza ya mshahara Kenya
Kasinge wa Nkulu ni kiongozi wa idara hiyo, amesema wanalifanyia kazi swala hilo katika jimbo lao la Tanganyika na ndio maana wanawaomba waajiri wakkati wowote wawape wafanyakazi wao vitendea kazi vya kujikinga .
Watu milioni 2 hufariki kwa mwaka kutokana na majeraha kazini
Takwimu za mashirika la Afya ulimwenguni (WHO) na ya wafanyakazi ILO katika ripoti yao ya pamoja wanakadiria kuwa magonjwa yanayohusiana na majeraha kazini yanasababisha vifo vya watu takribani milioni 2 kwa mwaka.